Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Ismail Ali Ussi, amepongeza kazi ya iliyofanya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Uongozi mzima wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Menans Komba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Elizabeth Mathias Gumbo kwa kujipanga sawa sawa katika kuukaribisha Mwenge wa Uhuru.
Ussi ameyasema hayo leo Mei 11, 2025 wakati wakikabidhi Mwenge wa Uhuru 2025 Mwenge wa uhuru 2025, wenye kauli mbiu isemayo “ jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu” kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, baada ya kuzunguka Zaidi ya Km 115, na kukagua Miradi 11 yenye thamani ya Zaidi ya Bilion 1.9 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Mwenge wa uhuru 2025, uliingia Halmashauuri ya Wilaya ya Songea Jana Mei 10, 2025 na umetembea jumla ya km 115.8, na kukagua jumla ya Miradi 11, yenye thaman ya zaid ya bilion 1.9 Katika miradi hiyo, Miradi 6, imekaguliwa, miradi 2 imezinduliwa, Mradi 1 umewekewa jiwe la msingi mradi 1 ugawaji wa Vyandalua kwa ajili ya kujikinga na Maralia na mradi mmoja ni kugawa majiko ya gesi.
“ Wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya songea, niwapongeze sana kwa kweli mmeupa hadhi na heshima mwenge huu wa Uhuru, kwanzia kwenye maandalizi, matembezi, Hamasa, nyaraka pamoja jinsi mlivyojitokeza kwa wingi kwenye viwanja kwa mkesha pale Magagura. Mmempa heshima Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan”
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Songea, Ndg. Ismail Ali Ussi ameyataja mambo matatu muhimu wanapaswa kuyazingatia katika kipindi hiki “ Ndugu wananchi naomba niwape mambo matatu mnapaswa kuyafanyia kazi, Moja hakikisheni mnashiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, pili Nendeni mkamheshimishe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa matumaini aliyowapatia wananchi wa Songea na Tatu WanaSongea Mmekua na Amani na Utulivu, na Mwenge wa Uhuru umeacha Amani na Utulivu, niwasihi sana, endelezeni Amnani hii na Utulivu.
Aidha mkimbiza mwenge amepongeza jitihada zinazofanywa na viongozi wa Halmashauri katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa