• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

KILIMO, MIFUGO NA UVUVI

HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

 

DIVISHENI YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI

   1 UTANGULIZI

Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 73 ambapo kati yao watumishi 13 wako  Makao Makuu na watumishi 60 wapo ngazi ya Vijiji na  Kata

Divisheni  inaundwa   na  vitengo  vitatu (3) ambavyo ni :

  • Kilimo
  • Mifugo
  • Uvuvi

2. MAJUKUMU YA DIVISHENI YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI

Jukumu kuu la divisheni hii ni kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Serikali kuu na Wadau kutoka Sekta binafsi. Divisheni hii ina sehemu tatu ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Shughuli za kila sehemu ni kama ifuatavyo:

2,1, Majukumu ya  Kitengo cha Kilimo

  • Kuandaa mipango na bajeti ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya Kilimo
  • Kusimamia sera na sheria mbalimbali zinasimamia kilimo katika ngazi ya Halmashauri
  • Kuratibu , Kutathimini na kufuatilia shughuli za huduma za ugani katika Halmashauri
  • Kusimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya kilimo, kwenye Halmashauri  ikiwepo  miundombinu ya umwagiliaji, maghala na masoko ya mazao ya wakulima
  • Kuwajengea uwezo wakulima juu ya uzalishaji wa tija, usimamiazi na uendeshaji wa miradi ya maendeleo.
  • Kuhamasisha matumizi ya zana bora za kilimo na teknolojia mbalimbali za kilimo zilizotokana na utafiti
  • Kushirikiana na wadau mbalimbali wanaojihusisha na maendeleo ya sekta ya kilimo ngazi ya Halmashauri
  • Kuainisha maenneo yanayofaa kwa kilimo pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo zilizopo katika  Halmashauri
  • Kufanya tathimini ya hali ya chakula katika  Halmashauri
  • Kuandaa taarifa na takwimu mbalimbali za maendeleo ya kilimo na Ushirika
  • Kuhimiza na kuhamasisha uanzishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika vyenye nguvu za kiuchumi na endelevu.
  • Kufanya ukaguzi kwa vyama vyote vya ushirika kwa lengo la kuhakiki  utunzaji wa kumbukumbu , Usahihi katika uandishi wa vitabu vya fedha ,Utunzaji wa fedha , Ongezeko la wanachama , n.k
  • Kuwajengea uwezo viongozi wa Bodi za vyama vyote vya ushirika yaani (SACCOS,AMCOS, na vyama vingine kwa lengo la kuongeza umahiri katika utendaji wao wa kazi.
  • Kupitia makisio ya mapato na matumizi ya vyama vya ushirika na kuwasilisha kwa Mrajis Msaidizi wa vyama vya ushirika (M) kwa lengo la kupitisha makisio hayo ili kuepusha chama kutumia fedha nje ya mapango ulio kusudiwa
  • Kusimamia chaguzi za viongozi wa vyama vya ushirika

2.2. Majukumu ya Kitengo cha Mifugo

  • Kutafsiri Sera,miongozo,sheria, na kanuni zinazo husiana na mifugo
  • Kuhamasisha wadau mbalimbali kama asasi zisizo za kiserikali,makampuni ya biashara, na wadau wengineo kuwekeza katika sekta ya mifugo
  • Kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo.
  • Kuandaa taarifa  mbalimbali za mifugo  na kuziwasilisha katika ngazi mbalimbali za Halmashauri,Mkoa na Taifa
  • Kutoa elimu kwa wafugaji juu ya kufuata mbinu bora za ufugaji
  • Kudhibiti magonjwa ya mifugo kwa njia ya tiba, uogeshaji na chanjo.
  • Kusimamia miundombinu ya mifugo kama vile machinjio, majosho na Minada
  • Kusimamia usafirishaji wa mifugo na mazao yake nje na ndani ya Halmashauri
  • Kuboresha  koosafu za mifugo kwa njia ya uhimilishaji
  • Kukusanya takwimu za mifugo kwa ajili ya mipango mbalimbali kwa serikali na wadau
  • Kutafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali.
  • Kukagua maduka /vituo vinavyotoa huduma za mifugo katika sekta binafsi 

2.3. .Majukumu ya Kitengo cha Uvuvi 

  • Kusimamia  sera,  miongozo , sheria  na kanuni za Uvuvi
  • Kutoa leseni mbalimbali za uvuvi na kukusanya mapato stahiki
  • Kudhibiti uvuvi haramu kwa kufanya doria  katika maeneo ya mialo na kuimarisha ulinzi wa rasilimali za uvuvi kupitia vikundi vya BMU ili kuwa na uvuvi endelevu.
  • Kuhamasisha kwa kutoa  elimu na ushauri juu ya  ufugaji wa samaki  kwenye mabwawa kwa lengo la kuinua kipato na lishe


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KULA YAMEANZA SONGEA DC

    April 29, 2025
  • MHE . JENISTA MHAGAMA AZINDUA MADARASA 27 NA VYOO MATUNDU 44, SONGEA DC

    March 16, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa