• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma akabidhi pikipiki 20 kwa maafisa Tarafa

Tarehe ya Kuwekwa: May 12th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekabidhi Pikipiki 20 kwa maafisa Tarafa wa Mkoa wa Ruvuma ikiwa ni  utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt.John Magufuli aliyoitoa Ikulu mwaka 2019 katika kikao cha maafisa tarafa wote nchini..

Akizungumza  kabla ya kukabidhi pikipiki hizo, Mndeme amemshukuru Rais kwa upendo ambao haujawahi kutokea tangu nchi yetu ipate Uhuru  kwa kiongozi wa juu wa Taifa kukaa kikao Ikulu na maafisa Tarafa wote nchini.

 Amelitaja lengo la kutoa pikipiki hizo ni kuhakikisha shughuli za maendeleo kwa maafisa tarafa zinafanyika kwa viwango vinavyotakiwa na kuona uchumi wa wananchi unaimarishwa ipaswavyo.

Amesema pikipiki hizo zinagawanywa katika wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma ambapo wilaya songea imepata pikipiki nne, Mbinga tano,Nyasa mbili,Tunduru saba na  Namtumbo mbili.

 “Pikipiki hizi mnapewa kusaidia katika kurahisisha mawasiliano kati ya ngazi ya kata na Halmashauri kwa upande mmoja na Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa upande mwingine,pikipiki hizi zitunzwe ili ziweze kudumu kwa muda mrefu’’,alisisitiza Mndeme.

Amewaagiza Maafisa Tarafa wafuatilie na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao na kuhakikisha wanasimamia ulinzi na usalama katika kata zilizomo ndani ya Tarafa husika.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Steven Ndaki amesema pikipiki hizo zilizotolewa na Rais Dkt.John Magufuli ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa maafisa hao walipokuwa Ikulu mjini Dar es salaam.

Akizungumza kwa niaba ya maafisa tarafa waliopata pikipiki hizo,Afisa Tarafa wa Songea mjini Mashariki Agustino Chazua  amempongeza Rais Dkt.John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake kwa maafisa tarafa.

Amesema hivi sasa pikipiki hizo zitawasadia kutekeleza majukumu yao kwa asilimia 100 ambapo watahakikisha wanakwenda kusikiliza kero mbalimbali kwa wananchi katika vijiji vyote .

Matangazo

  • WAKALA WA KUKUSANYA USHURU WA MAZAO NDANI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA January 06, 2021
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji July 23, 2018
  • TANGAZO LA KUUZA VIWANJA June 03, 2019
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • HAKUNA mwanafunzi atakateye baki nyumbani 2021

    January 13, 2021
  • "WATUMISHI wa umma zingatieni uadilifu kwenye kazi ",amesema Mwakipesile

    December 30, 2020
  • WANAFUNZI wote 2082 waliochaguliwa kidato cha kwanza Songea kuanza masomo Januari

    December 28, 2020
  • DC aagiza RUWASA kutoa Elimu kwa wanachi kuhusu umuhimu wa vyanzo vya maji

    December 17, 2020
  • Ona Zote

Video

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akagua mradi wa maji Peramiho
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa